IQNA

Kiongozi Muadhamu atoa msamaha kwa  wafungwa zaidi ya 3,000 kwa mnasaba wa maadhimisho ya Mapinduzi ya Kiislamu

15:40 - February 06, 2025
Habari ID: 3480169
IQNA – Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ameidhinisha kusamehewa kikamilifu au sehemu ya adhabu wafungwa zaidi ya 3,000 katika maadhimisho ya mwaka wa 46 wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Jamhuri ya  Kiislamu ya Iran  imesema, alikubali siku ya Jumatano kutoa msamaha au kupunguza adhabu za wafungwa wa Iran kufuatia pendekezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mahakama, Hujat-Al-Islam Gholam Hossein Mohseni Ejei, ambaye aliomba msamaha wa Kiongozi kwa wafungwa waliotimiza masharti maalum.

 Jumla ya wafungwa 3,126 walipata msamaha huo.

Katika barua yake, Hojat-ol-Islam Mohseni Ejei aliomba msamaha huo kwa mnasaba wa siku tukufu za Eid al-Mab’ath, Idi za mwezi wa Shaaban katika kalenda ya Hijria, na kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kifungu cha 110 cha Katiba kinampa Kiongozi mamlaka ya kutoa msamaha au kupunguza adhabu za wafungwa kwa mapendekezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mahakama.

Mapinduzi ya Kiislamu Yalivunja Ushawishi wa Madikteta: Mkuu wa Mahakama ya Iran

Hata hivyo, msamaha huu hauwahusu wafungwa wa makosa fulani, ikiwa ni pamoja na wale waliopatikana na hatia ya:

Usafirishaji haramu wa dawa za kulevya kwa kutumia silaha

Biashara haramu ya silaha

Utekaji nyara

Mashambulizi ya tindikali

Ubakaji

Uporaji wa kutumia silaha

Rushwa

Ubadhirifu wa mali ya umma

Utengenezaji wa fedha bandia

Utakatishaji fedha

Uvurugaji wa uchumi

Usafirishaji wa pombe

Magendo ya bidhaa kwa mtandao wa uhalifu uliopangwa.

 

3491761

 

 

Kishikizo: kiislamu
captcha